Msemaji
Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, ameongoza shughuli ya arobaini ya
Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya
mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole
Maitei, iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha
Vijijini katika mkoa wa Pwani.
Katika
shughuli hiyo ambayo ilifanyika kimila, Sendeka ambaye alialikwa
kuongoza shughuli hiyo Kama kiongozi wa Kimasai anayeheshimika,
aliwataka Jamii ya Wamasai Kanada za mikoa hiyo, kuwa na Umoja na
kutumia hekima na busara katika kumpata mrithi wa nafasi iliyoachwa na
Chifu Ole Maitei.
Aliwataka
kumteua Chifu au Laiboni, mwenye sifa zinazostahili ambazo hata kama
Chifu Ole Maitei angekuwepo angerithika kuwa anafaa kuwa mrithi wake.
Kwa
heshima aliyopewa katika shughuli hiyo Ole Sendeka, aliweka kwenye
kaburi kibuyu na usinga ambavyo ni vifaa alivyokuwa akitumia Chifu Ole
Maitei ambaye ndani ya Jamii hiyo anatambuliwa zaidi kwa cheo cha
Laiboni ambaye ni kiongozi mkuu wa viongozi wanaofuatia hadhi yake
wanaoitwa Laigwanani.
Uwekaji vifaa hivyo ulifayika huku ukishuhudiwa na
ndugu jamaa na wanajamii hiyo, Mjane na Dada wa Marehem.
Mmoja
wa Malaigwanani waliohudhuria shughuli hiyo, alisema, Kibuyu hicho
alichoweka Ole Sedeka kwenye kaburi, ndani kilikuwa na mawe ambayo
Chifu Ole Maitei alikuwa akiyatumia kubashiri yanayoweza kutokea mbele
ya safari huku usinga akiutumia kupungia kuwasalimia wageni au kufukuzia
mbali mifarakano na balaa katika jamii yao.
Kabla
ya kuweka vifaa hivyo kwenye kaburi, Sendeka alitanguliwa na watoto
wote wa kiume kumwaga kwenye kaburi hilo asali, maziwa ya ng’ombe na
mafuta ya kidari cha dume maalum la ng’ombe kama ishara ya kutekeleza
mila na desturi.
Chifu
Ole Maitei ambaye alikuwa kiungo muhimu kwa kuunganisha jamii hiyo ya
Kimasai hasa katika utatuzi wa migogoro yawafugaji kutoka jamii hiyo na
wakulima katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro,
Mbeya na Iringa alipokea nafasi ya Uchifu kutoka kwa Laibon Labani
Moreto ambaye alifariki miaka ya 2005.
0 comments:
Post a Comment