Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein, amefuta uteuzi wa Naibu Kamishna wa Bodi ya Mapato
Zanzibar (ZRB), Hafidh Ussi Haji.
Nafasi yake imechukuliwa na Khadija Shamte Mzee, ambae uteuzi wake
umefanywa chini ya uwezo aliopewa Rais na kifungu cha 15(1) (A) cha
sheria ya Bodi ya Mapato ya mwaka 1996 kama ilivyorekebishwa na kifungu
cha 11 cha sheria namba 2 ya mwaka 2000.
Aidha Dk. Shein, amemteua Amour Hamil Bakari kuwa Kamishna wa Bodi
ya Mapato Zanzibar kuchukua nafasi ya Abdi Khamis Faki ambaye anastaafu
kwa mujibu wa sheria.
Uteuzi wake umeanza Agosti 1,2016 huku uteuzi wa Naibu Kamishna ukianza Julai 25, 2016.
Dk. Shein pia amemteua Umi Aley kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali, uteuzi ambao ameufanya
chini ya kifungu cha 11(a) cha sheria namba 11 ya 2008 iliyounda Shirika
hilo.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia
Facebook
,
Twitter na
Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment