Mwenyekiti Mstaafu CCM,Dr.Jakaya Mrisho Kikwete.
Mapokezi makubwa yameandaliwa leo wilayani Bagamoyo kumpokea
Mwenyekiti mstaafu wa
Chama Cha Mapinduzi(CCM),
Dkt. Jakaya Kikwete baada
ya kufanikiwa kukitumikia Chama cha Mapinduzi vizuri.
Kwa mujibu wa Katibu Mwenezi wa CCM, Wilaya ya Bagamoyo,Kassim Gogo
alisema kuwa
mapokezi hayo yataanzia Chalinze hadi Bagamoyo. Alisema kuwa wanaCCM wa
wilaya hiyo wanajisikia furaha sana kuona Jakaya
Kikwete ambaye ni mzaliwa wa Kijiji
cha Msoga, wilayani humo,
ameng’atuka salama baada ya kukitumia chama na serikali
kwa miaka kumi.
Gogo, alisema kuwa katika mapokezi hayo watakuwepo madiwani wote wa
wilaya hiyo,
viongozi wa CCM, wabunge wote wa Mkoa wa Pwani na wananchi.
Aliongeza kuwa wakati wa hafla hiyo pia Mwenyekiti mstaafu, Kikwete
atakabidhiwa zawadi
mbalimbali ikiwemo kumvisha gwanda ili awe mlezi wa
CCM Mkoa wa Pwani.
Katika sherehe za mapokezi zitakazofanyika mbele ya Makao Makuu ya Ofisi
za
CCM za wilaya hiyo zilizopo Bagamoyo Mjini, patakuwepo ngoma za
asili ya makabila ya
Wakwere, Wazaramo na Wazigua pamoja na wasanii
mbalimbali.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia
Facebook
,
Twitter na
Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment