JAKAYA
Kikwete, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) anayemaliza muda wake
amemtahadharisha mwenyekiti mtarajiwa wa Chama hicho John Magufuli kwa
kumweleza kuwa uenyekiti ndani ya CCM siyo lelemama kwani wajumbe
wasipoelewa wanachokitaka.
Mbali na kumpa tahadhari hiyo pia alikiri kuwa mwaka jana chama hicho kilikumbwa na misukosuko mingi ambayo ingeweza kukifanya chama hicho kuanguka kwani kilikuwa na mafisi wengi ambao walikuwa wakisubiri mkono udondoke ili washibe
Ametoa
kauli hiyo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya
chama hicho ambayo ajenda ilikuwa moja tu ya kujadili na kupitisha jina
la mwenyekiti ambalo litapelekwa katika mkutano mkuu kwa lengo la
kupigiwa kura.
Kikwete amesema ..."CCM
ilikuwa ivunjike wakati wa kipindi kigumu cha uchaguzi wa mwaka jana
lakini tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumeweza kukaa imara na kukitafa
chama kutovunjika.
“Tunasema
kikao kama hiki hatumwi mtoto tunakuja wenyewe kikao cha leo ni kikao
cha kihistoria, kwa mamna mbili kwanza ni kikao changu cha mwisho,
nikija kwenye NEC ni pale mtakapo nialika lakini tulikubaliana kwamba
wazee hao wameishatumikia vya kutosha na tuwaache wapumzike utaratibu wa
hapo nyuma ukimaliza uenyekiti unakuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu
na halmashauri kuu.
“Siku
moja Mzee Mkapa akasema bwana mbona sisi wazee mnatusumbua sana
mnatuita kila siku na sisi tumeishakuwa wazee tunakaa mpaka saa saba
usiku kwa hivi sasa tuacheni, ndipo niliposema hatuwezi na tukaamua
kuunda baraza la wazee.
“Tukaona
hatuwezi kuwaita kila siku lakini tunawatengenezea baraza la wazee
ambalo ni baraza la ushauri kimsingi linahitajika kwa jambo muhimu sana
kama ilivyo kuwa mwaka lakini nilijadiliwa nikaambiwa JK hataki wazee
lakini nikasema huo ni uamuzi wa busara kabisa” amesema Kikwete.
“Kuna
maswala makubwa ya chama chetu na uhai wake kama ilivyokuwa mwaka wa
jana, eeee chama chetu kilikuwa kimekaa katika msukosuko mkubwa mnaingia
hapa watu wanaimba hiki wanaimba kile mjadala mkali lakini nikasema
tutavuka tu maadamu tupo ndiyo changamoto ya uongozi.
“Na
maadamu CCM haikuvunjika mwaka wa jana haitavunjika tena, maana mafisi
yalikaa hapa yanasubiri mkono udondoke lakini haukudondoka na maadam
haukudondoka mwaka wa jana CCM haidondoki,”amesema Kikwete.
Amesema
rais atakuwa mwenyekiti na wakati mwingine kuna wakati kikao kinakuwa
kigumu kwani wajumbe wanataka kutendewa haki wa wasipopata haki zao
wanakuwa wakali sana.
Amesema
halmashauri kuu ni kikao Muhimu cha uongozi pale ambapo hakuna mikutano
ya chama amesema kamati kuu ni kikao cha kusimamia shughuli muhimu za
chama na NEC ni kikao cha juu cha kutoa viongozi.
Amesema
wajumbe wa vikao ni wepesi sana kusifia lakini wanakuwa wakali sana
pale ambapo mambo yanaenda vibaya hivyo kiongozi ni lazima kumsikiliza
na kujua nini ambacho wajumbe wanataka.
Amesema
wajumbe hao wanakuwa wakali kwa kuwa wanataka mambo ndani ya chama
yaende vizuri ili nao ndani ya chama waweze kujivunia.
Mbali na hayo amesema wajumbe wanatakiwa kushirikiana na mwenyekiti mpya ili kukifanya chama kuweza kusonga mbele zaidi.
0 comments:
Post a Comment