SERIKALI
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo imetiliana saini na Benki ya
Exim ya China makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango
cha kisasa (Standard Gauge).
Makubaliano
hayo ya awali yamefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango
Dkt. Servaciaus Likwelile kwa niaba ya Tanzania na Naibu Meneja Mikopo
Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya utiliaji saini Dkt. Likwelile amesema hatua hiyo
inawezesha hatua za upembuzi yakinifu, usanifu na uundwaji wa timu za
pamoja kuanza kuanisha mahitaji halisi ya ujenzi wa mradi huo.
Zaidi
ya Shilingi Trilioni 16 za Tanzania zinatarajiwa kutumika katika ujenzi
wa mradi wa reli ya kati yenye urefu wa Kilometa 2,190 ambapo Benki
hiyo itashirikiana na Serikali ya Tanzania katika ujenzi wake.
Mradi
wa ujenzi wa reli ya kati utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha
kisasa kutoka Dar es Salaam-Tabora-Isaka-Mwanza na
Tabora-Mpanda-Kalemela-Uvinza-Kigoma-Isaka-Keza hadi Msongati.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
0 comments:
Post a Comment