Jux amedai kuwa kamwe hatoacha kufanya kazi na Nahreel, kwakuwa ndiye
producer wa muziki aliyemtengenezea wimbo wake wa kwanza uliofanya
vizuri Afrika nzima.
Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa wasanii wengi waliokuwa
wakifanya kazi na Nahreel wakiwemo Weusi wameikimbia studio yake ya The
Industry baada ya kubadilisha utaratibu wa kurekodi nyimbo.
Jux kwa upande wake amekanusha na kudai kuwa Nahreel bado ni mshkaji
wake mkubwa na mwishoni mwa wiki walikuwa pamoja. Anadai kuwa bado ana
kazi nyingi kwa producer huyo na kwamba wakati mwingine huamua
kubadilisha ladha ili kuogopa nyimbo zake kuzoeleka.
“Nahreel mimi amenitolea hit song, amenitolea ‘Looking For You,
naweza kusema ndio wimbo ambao hata Kiafrika ndio ilifanya poa sana,”
Jux ameimbia Bongo5.
“Hata kuna wasanii wakubwa wa Kiafrika wengine ambao siwezi kuwasema
sasa hivi wameiskia na wameniona huku na tunakuja kufanya nao nyimbo
baadaye, ni sababu ya Looking For You. Nisingetoka kwa Bob labda
nisingepata kitu tofauti,” amesisitiza.
Kingine amedai kuwa muda wote huu hakuwepo alikuwa nchini China na
pia Nahreel amekuwa na miradi yake mingine mingi ikiwemo kwenda Afrika
Kusini kufanya video za Navy Kenzo na za wasanii wa The Industry.
“Karudi, tumekutana jana, bado mshkaji wangu na bado nafanya naye
kazi pia, sababu ya yeye kubadilisha utaratibu wa studio mimi
haijaniathiri chochote kwasababu ni program zake yeye mwenyewe alizotaka
kufanya, kwahiyo mimi naona ni sawa.
Kwanza mimi ni mmoja wa watu
niliyeona hivyo yaani Nahreel alikuwa anadeserve hicho kitu pia
kwasababu alikuwa anafanya kazi sana.”
Home / News
/ Nahreel alinitengenezea hit yangu ya kwanza Afrika, siwezi kuacha kufanya naye kazi – Jux
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment