NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

SAKATA LA WAJASIRIAMALI WILAYA YA BUNDA YACHUKUA SURA MPYA.

 BUNDA

Sakata la kuondolewa wafanyabiashara wadogo wadogo katika genge la Asubuhi na la jioni katika mji wa bunda mkoani Mara limezidi kuchukua sura mpya mara baada ya baadhi ya viongozi wa serikali ngazi ya kata kuonekana kupita katika maeneo hayo wakiwa na askari mgambo wakitaka wafanyabiashara hao kuhama.

Wakizungumza kwa jazba jana katika maeneo yao ya biashara wajasiriamali hao wamesema kuwa kuhamishwa kwao katika maeneo hayo ni kuwaonea kwakuwa ni sehemu walizopewa kihalali, na kuongeza kuwa wanashangazwa na agizo hilo la viongozi wa serikali kwani katika mahali walikoelekezwa hapatoshi kutokana na uwingi wao.

Newspointtz ilizungumza na Diwani wa Bunda mjini mh, Joash Kunaga katika eneo hilo la wafanyabiashara na kueleza kuwa suala hilo linatokana na taarifa walizozipata zinazodai kuwa ccm ndio wanaotaka kumilika eneo hilo jambo linalopelekea wananchi hao kufanya shughuli zao kwa shida.

Hata hivyo kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bunda Lidya Bhupilipili alisema kuwa wafanyabiashara hao walishapewa muda wiki mbili zilizo pita na wanapaswa kuondoka katika maeneo hayo kwa utarabibu .

Pamoja na hayo taarifa ambazo hazijathibitika zinaeleza kuwa wafanyabiashara hao leo wameonekana wakitoka katika ofisi za mkurugenzi wa mji huku wakiwa na tabasam jambo linaloashiria kuwepo makubaliono ya utata uliokuwepo mwanzo.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment