NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Video: ‘ZOMBI’ LA TEMEKE MARKET LILIVYOTAFUNA NYAMA YA FARU JEURI

Temeke Market wamekata tiketi ya kwenda hatua ya nusu fainali ya michuano ya Sports Extra Ndondo Cup kwenye mchezo war obo fainali ya kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Chuo cha Utalii au Bandari lakini ukifahamika pia kama Wembley. Faru Jeuri ambao walikuwa mabingwa watetezi watetezi wa kombe hilo wametupwa nje ya michuano kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 bao lililowekwa kambani na Ramadhani Madebe dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza na kudumu hadi dakika ya mwisho. Angalia video ujionee zombi la Market lilivyokula nyama mbichi ndani ya uwanja wa Bandari
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment