NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

CRISTIANO RONALDO MCHEZAJI BORA WA ULAYA

ronn
Cristiano Ronaldo amewashinda wwachezaji Antoine Griezman na Gareth Bale na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya kwa upande wa wanaume. Ushindi huu umetokana na mafanikio yake msimu uliokwisha huku akiwa ametwaa vikombe vikubwa vya ulaya kwa maana klabu bingwa ulaya na kombe la mataifa ya Ulaya.
Ronaldo pia alikuwa mfungaji bora wa Ulaya huku akiwa wa pili kwa ufungaji katika ligi kuu ya nchini Hispania. Ikumbukwe pia, Ronaldo alifika fainali hizi huku mpinzani wake akiwa ni Antoine Griezman na kumshinda kote ijapokuwa kwenye fainali ambayo Ureno walitwaa ubingwa aliumia mapema sana.
Ronaldo alifunga mabao 51 kwenye mechi 48 msimu uliopita huku akifunga mabao 3 pekee kwenye mashindano ya mataifa ya Ulaya ambapo mchezaji Antoine Griezman alikuwa mfungaji bora.

Yaome maswali na majibu aliyoyajibu Ronaldo baada ya kutwaa tuzo hiyo huku pia akiwapongeza wachezaji wenzake waliofika kwenye hatua ya mwisho ya kinyang’anyiro hiki, Bale na Griezman.
RONA
Katika hatua nyingine mchezaji Ada Hegerberg ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ulaya kwa upande wa akina dada
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment