NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

WALIOCHUJWA UDOM KUSOMEA UALIMU SHULE ZA MSINGI

WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imewapangia vyuo vya serikali wanafunzi 1,450 ambao walikosa sifa ya kurudishwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) pamoja na vyuo vingine baada ya serikali kuwachuja na kuwarejesha wale waliokuwa wanastahili katika awamu ya kwanza.

Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Leornard Akwilapo alisema jana alipokuwa akitoa taarifa za ziada kuhusu wanafunzi waliokuwa wanasoma Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Sayansi chuoni Udom.udom (1)

Dk Akwilapo alisema kati ya wanafunzi hao 1,450, 290 walikuwa wanasomea programu ya Stashahada ya Ualimu wa Sekondari na 1,181 walikuwa wakisoma programu ya Stashahada ya Ualimu wa Msingi.

“Wanafunzi waliokuwa wanachukua Stashahada ya Ualimu wa Sekondari na kukosa sifa ni 290. Kati yao hawa, wanafunzi 269 walikuwa na daraja la kwanza hadi la tatu, hawa tumewapangia kuanza masomo ya ualimu wa shule za msingi. Hawa watakuwa katika Chuo cha Mtwara kawaida. Katika kundi hili wanafunzi 21 hatujawapangia kwa sababu wana daraja la 1V,” alisema Dk Akwilapo.

Alisema wanafunzi hao 1,181 waliokuwa wanachukua Stashahada ya Ualimu wa Msingi waliagizwa waombe mafunzo watakayoona yanawafaa kulingana na ufaulu wao kupitia Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment