NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

LEMA ABISHANA NA POLISI WA MAHAKAMANI

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amezua tafrani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, baada ya askari polisi waliomleta awali kutaka apande gari kwenda mahabusu kwa sababu ya kutokidhi masharti ya dhamana.

Awali, Lema alisomewa makosa mawili yaliyokuwa yakimkabili mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Desdery Kamugisha na Wakili wa Serikali, Innocent Njau.

Katika mashtaka ya kwanza ni la kutuma ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwake kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. Mashtaka ya pili, kutumia Whatsapp kwa ajili ya kuwashawishi wananchi wa Jiji la Arusha, kuandamana Septemba mosi.LEMA

Baada ya Lema kusomewa mashtaka hayo, Hakimu Kamugisha alimuuliza kama ni kweli au la; na Lema alikana. Baada ya kukana, wakili Njau aliomba Lema asipewe dhamana kwa sababu wana taarifa za kiintelijensia kuwa endapo atapewa dhamana, usalama wake utakuwa mashakani.

Saa 8:20 mchana askari polisi walimtoa chumba cha mahabusu na kutaka kumpandisha gari la Polisi kwa ajili ya kumpeleka mahabusu Kisongo. Kutokana na sintofahamu hiyo, Lema alibishana na polisi hao, huku akiwa na mawakili wake, Mallya na James Lyatuu, waliohoji kuwa wanampeleka wapi wakati muda wa mahakama haujafika.

“muda wa mahakama haujafika mnanipeleka wapi, nasema nitafia hapa mahakamani, saa hizi ni saa 8:00 muda wa mahakama haujaisha, mnanipeleka wapi, siendi, mniue, siendi popote, mniue hapa hapa, muda wa mahakama haujaisha, ‘broo’ mnanipeleka wapi na kwa nini mnanifanyia hivi, nasema siendi kokote, bora kufa, sikubali” alisema Lema.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment