Madiwani watatu wa Chadema na mfuasi
mmoja wa chama hicho wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Rombo kwa
makosa ya kufanya uchochezi.
Madiwani hao, Nicolaus Kimario (Kirio),
Anasia Kimario (Viti Maalumu), Daud Tarimo (Leto )na mfuasi wa Chadema,
Rogath Kanje walikana mashtaka hayo.Mwendesha
mashtaka, Bernard Machivya ameieleza mahakama kuwa washtakiwa walitenda
kosa hilo Agosti 25, wakiwa nyumbani kwa mmoja wa washtakiwa Nicolaus
Kimario.
Amedai kuwa washtakiwa walitenda kosa
hilo kwa pamoja wakati wakifanya vikao vya kuhamasisha wananchi
wajitokeze kwenye maandamano ya Ukuta Septemba Mosi.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya
ya Rombo, Naomi Mwerinde ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 5 na
watuhumiwa wote wataendelea kukaa rumande.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
MADIWANI CHADEMA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UCHOCHEZI
Reviewed by Newspointtz
on
08:22:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment