UFARANSA imesema itaongeza mchango wake
katika kuendeleza sekta mbalimbali nchini kutoka wastani wa Euro
milioni 50 kila mwaka, ambazo huzitoa kupitia shirika lake la maendeleo
la AFD.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo
ya Nchi za Nje na Maendeleo ya Kimataifa wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault
ambaye alifanya ziara nchini na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga.
Waziri huyo akiwa nchini pia alifanya
mazungumzo na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli. Katika
mazungumzo yake na Dk Mahiga, Waziri huyo alisema uhusiano kati ya
Ufaransa na Tanzania uliodumu kwa muda mrefu utaendelea kuimarishwa.
Aidha
Ayrault aliipongeza Tanzania kwa kuendelea kupigania amani na usalama
katika bara la Afrika na hasa juhudi zake za mara kwa mara za
kuhakikisha kunapatikana suluhu kwa migogoro ya nchi za Maziwa Makuu.
Aliipongeza Tanzania kwa kukubali
kupokea maelfu ya wakimbizi kutoka Burundi na kuwahifadhi na pia mchango
wake katika kukabiliana na ugaidi duniani.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
Ufaransa waahidi neema Tanzania
Reviewed by Newspointtz
on
08:21:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment