NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

UMMY awaonya wala kuku na mayai ya kuku

 

Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa nchini, TFDA, imebaini uwepo wa kemikali zinazobakia kwenye mayai ya kuku na kuku ambao tayari wanaenda kuuzwa ambazo si salama kwa afya ya binadamu.

Hayo yanebainika wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya washauri wa TFDA ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ameiagiza mamlaka hiyo kuchukua sampuli na kufanya vipimo ili wizara ichukue hatua na kunusuru afya za watumiaji wa vyakula hivyo.

Katika hatua nyingine, Mh. Ummy ameiagiza TFDA kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye viwanda vya dawa kwa kuwapatia wataalam ambao watahakikisha dawa zinazozalishwa nchini zina ubora, kwani hivi sasa zaidi ya asilimia 85 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya ushauri ambayo inaishauri wizara kutoka TFDA Dkt. Ben Moses amesema wameyapokea maelekezo ya waziri na watayatekeleza kwa kipindi kifupi kuanzia leo, hasa suala la usalama wa chakula na dawa kuzingatiwa.


Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment