Mahakama
ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu Ally Rashid maarufu kwa
jina la Ally Mwizi kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na
hatia ya kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka 25, makaburini.
Hukumu
hiyo iliyovuta hisia za watu wengi wa Manispaa ya Mpanda ilitolewa jana
na Hakimu wa mahakama hiyo, Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na
ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka pasipo kutia shaka,
ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi, Jamila Mziray.
Awali
Mwendesha Mashtaka Mziray alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo
alitenda kosa hilo Juni 17, mwaka huu, saa 2:00 usiku katika makaburi ya
Kashaulili yaliyoko katika Mtaa wa Kotazi, Manispaa ya Mpanda.
Ilidaiwa
kuwa mshtakiwa kabla ya kutenda kosa hilo alimfuata msichana huyo
ambaye alikuwa ameibiwa vitu vyake vya ndani ya nyumba ambapo
alimdanganya kuwa ana uwezo wa kumsaidia kuvipata vitu vyote
alivyoibiwa.
Mziray
alidai kuwa baada ya msichana huyo kuahidiwa na mshtakiwa kuwa vitu
vyake alivyoibiwa vitapatikana alimlipa mshtakiwa Sh 30,000 ili
akamwoneshe vitu vyake alivyoibiwa.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa siku hiyo ya tukio mshtakiwa alimpigia simu
msichana huyo saa 2:00 usiku akimtaka waonane ili akamwonesha vitu vyake
vilivyoibiwa.
Mziray
alieleza mshtakiwa alikwenda nyumbani kwa msichana huyo na wakaongozana
hadi kwenye makaburi ya Kashaulili ambako alidai ndiko vilipo vitu
vilivyoibwa lakini ghafla mshtakiwa alimpiga ngwala msichana huyo na
kumbaka na kumlawiti huku akimtishia maisha iwapo akijaribu kupiga
kelele.
“Baada
ya kumtendea unyama msichana huyo, mshtakiwa alimwomba dada huyo waende
kwenye nyumba ya kulala wageni inayoitwa Kingi Paris ili wakaendelee
kufanya mapenzi zaidi kwa kile alichodai kuwa nyumba hiyo ya wageni
inafaa zaidi kufanyia tendo la ndoa kuliko juu ya kaburi,” alidai.
0 comments:
Post a Comment