RAIS John Magufuli amepokea taarifa ya
maafa yaliyosababishwa na tetemoko la ardhi lililotokea katika mkoa wa
Kagera na mikoa jirani ya Mwanza, Geita na Kigoma kutoka kwa Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa
hiyo ya maafa na michango kwa ajili ya waathirika wa maafa hayo, Rais
Magufuli aliwashukuru wote waliojitoa kusaidia waathirika akiwataja
marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais wa Uganda,
Yoweri Museveni, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Rwanda, Paul
Kagame, kuwa wamempigia simu za kumpa pole na tayari wametoa misaada
yao.Taarifa
ya Ikulu iliyotolewa Dar es Salaam jana ilisema pamoja na kupokea
taarifa hiyo, Rais Magufuli alipokea mchango wa fedha taslimu Dola za
Kimarekani 200,000 sawa na takribani Sh milioni 437 kutoka kwa Rais
Museveni. Pia Rais Magufuli alipokea taarifa ya mchango wa mabati,
blangeti na magodoro vyenye thamani ya Sh milioni 115 kutoka kwa Rais
Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani
Kagera.
Pia alizishukuru nchi mbalimbali,
mashirika, wafanyabiashara, watumishi wa umma na watu binafsi
waliochangia na kusema michango hiyo ina umuhimu mkubwa katika
kukabiliana na athari za maafa haya.
Alitoa wito kwa Watanzania na wote
walioguswa na maafa hayo kuendelea kutoa misaada kwa waathirika kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, huku akionya na
kuvitaka vyombo vya dola kuwafuatilia watu wanaotaka kutumia maafa haya
kukusanya michango kwa lengo la kujinufaisha.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
MARAIS WA EAC WACHANGIA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA
Reviewed by Newspointtz
on
10:45:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment