NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Ben Pol asisitiza kuitoa album yake mwaka huu

Ben Pol amedai kuwa mpango wa kutoa album yake mwaka huu upo pale pale.
13649292_266385900403070_2002980860_n
Ameiambia Bongo5 kuwa album hiyo imechelewa kutoka kwasababu yeye na uongozi wake wanatengeneza mkakati wa kuipromote na kuiuza ili iende mbali na kumfikia kila shabiki aliyenuiwa.

Hata hivyo muimbaji huyo wa ‘Moyo Mashine’ amedai kuwa lengo la kuitoa si kupata fedha bali ana sababu zingine kuu mbili.

“Moja ni kutengeneza ukamilifu wa mwanamuziki,” anasema Ben.

“Mimi si mtu wa magumashi, kama unataka ukamilifu wa kuitwa mwanamuziki au msanii uliyekamilika, lazima uwe na album,” ameongeza.

“Lakini pili, nataka baadaye biashara ya album ikirudi kuwa stable, ikija kuwa ni deal yaani, niweze kuwa katika watu ambao walithubutu kutoa album licha biashara kuwa bado si nzuri, Ben Pol alikuwepo, kwahiyo niingie kwenye wale wanaharakati waliothubutu kurudisha biashara ya album regardless ya situation ya mauzo ya kipindi hicho au situation ya biashara yenyewe kwa ujumla.”
“Kwahiyo watu wategemee album yangu mwishoni mwa mwaka huu mzigo utatoka.!
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment