NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

BUNGE KUANZA NA MISWADA 6 NA MASWALI 110 KWA SERIKALI

MKUTANO wa Nne wa Bunge la 11 unatarajiwa kuanza leo mjini hapa, huku miswada sita ukiwemo wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari ukitarajiwa kuchukua nafasi kubwa.

Katika mkutano huo, wabunge wa kambi ya upinzani ambao walisusia siku kadhaa za mkutano uliopita, wamesema kwamba watahudhuria.bungeniMbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alithibitisha jana kwamba wabunge wa upinzani wataingia bungeni.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya Bunge kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, jumla ya maswali 110 yanatarajiwa kuulizwa na wabunge na kujibiwa na Serikali.

Aidha, Waziri Mkuu anatarajiwa kuulizwa maswali 16 ya papo kwa hapo. Taarifa hiyo ilisema miswada sita ya sheria iliyosomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Tatu wa Bunge na baadaye kupelekwa katika kamati husika ili ifanyiwe kazi, itaendelea kushughulikiwa katika hatua zinazofuata ikiwa ni pamoja na kusomwa kwa mara ya pili, kamati ya Bunge zima na kusomwa kwa mara ya tatu.

Miswada hiyo ni pamoja na ule wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari ya mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Utathmini na Usajili wa Wathamini wa mwaka 2016, Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serika wa mwaka 2016.

Pia utakuwepo Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Wanataaluma wa Kemia wa mwaka 2016, Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ya mwaka 2016.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment