BUNGE limeelezwa kuwa Rais John
Magufuli hajavunja sheria yoyote kwa kuzuia siasa za hovyo,
iliyotafsiriwa kuwa amefuta siasa nchini, bali kwa kufanya hivyo
ameiheshimu, ameihifadhi na kuilinda Katiba ya nchi.
Aidha, wanasiasa na watu wengine wanaodhani Rais amevunja sheria, wameshauriwa kwenda mahakamani au kudai majadiliano na Rais.Hayo
yalisemwa juzi jioni mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk
Harrison Mwakyembe alipokuwa anahitimisha mjadalaa wa Muswada wa Sheria
ya Upatikanaji wa Taarifa wa Mwaka 2016, aliouwasilisha bungeni na
kujadiliwa kwa siku mbili mfululizo.
Mwakyembe alilazimika kuyasema hayo
baada ya wabunge wa kambi ya upinzani, kuwashambulia waziri huyo na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kuwa hawaungi mkono muswada
uliowasilishwa bungeni kwa kuwa una nia ovu.
“Dk Mwakyembe huyu huyu ndiye
aliyetetea kauli ya Rais Magufuli ya kuzuia mikutano ya hadhara wakati
anajua inakubalika kikatiba,” alisema Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema aliyeungwa mkono na Mbunge wa Momba, David Silinde na Mchungaji
Peter Msigwa wa Iringa, wote wa Chadema.a
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
DK MWAKYEMBE- JPM HAVUNJI KATIBA YA NCHI
Reviewed by Newspointtz
on
08:58:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment