Producer Lamar amedai kuwa hadi sasa pengo la marehemu Geez Mabovu ni kubwa na anaendelea kulihisi.
Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Vibe la Kitaa cha ABM Radio ya
Dodoma, DJ Rodger, Lamar amesema Geez alikuwa zaidi ya msanii kwake.
“Geez Mabovu nilifanya naye kazi tangu naanza career yangu,
nimekutana naye nikiwa G Records kuanzia mwaka 2004 ingawa nilikuwa
namsikia kipindi cha nyuma, lakini kuanza kufanya kazi tulianza 2006
Bongo Records,” alisema Lamar.
“Geez toka amefariki kuna vitu vingi ambavyo navimiss kutokana na
Geez hakuwa sio artist kwangu, alikuwa kama ndugu yangu, mtu ambaye
alikuwa close na mimi, tunashare vitu vingi halafu kwao wananijua home
kwetu alikuwa anakuja kama nyumbani. Mpaka sasa hivi baba yake
nawasiliana naye,” ameongeza.
“Mwaka jana nilienda kwao kwenda kutembelea mpaka kaburi lake, kwahiyo kuna vitu vingi ambavyo nimevimiss kutoka kwa Geez.”
Lamar amesema rapper huyo aliacha album yenye nyimbo takriban 10 na kwamba anasubiria muda muafaka wa kuachia single ya kwanza.
Geez alifariki November 2014.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment