NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

KAULI YA JPM YA KUTAKA JECHA APEWE TUZO YAZUA TAFRANI CUF

 Image result for picha ya cuf

 

KAULI ya Rais John Magufuli, kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) Jecha Salim Jecha, anasitahili kupewa tuzo kwa kufanikisha uchaguzi wa marudio imewakera wanachama wa Chama cha wananchi (CUF).

 Image result for picha ya cuf

  Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salim Bimani Abdalla alisema chimbuko la mgogoro wa Zanzibar ni Mwenyekiti wa Zec huyo baada ya kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kinyume na Katiba na Sheria ya Uchaguzi.

Alisema katika uchaguzi huo ripoti za waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje, wakiwemo Umoja wa Ulaya (EU), Jumuiya ya Madola, Marekani na Uingereza walisema ulikuwa huru na wa haki.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment