Timu ya taifa Uganda imefuzu katika fainali za Kombe la Mataifa
Bingwa Afrika 2017 baada ya miaka 38, The Cranes walishinda 1-0 dhidi ya
Comoro siku ya Jumapili, ushindi ambao umewafanya kutimiza pointi 13
zilitosha kuwapa tiketi ya AFCON 2017.

Goli la Uganda limefungwa na Farouk Miya mbele ya mashabiki kibao wa Uganda jijini Kampala.
Mara ya mwisho The Cranes kucheza Afcon ilikuwa mwaka 1978
ilipofanikiwa kufika hadi fainali na kufungwa na Black Stars ya Ghana.
Mataifa 16 yatashiriki michuano hiyo itakayoandaliwa 14 Januari hadi 5 Februari. huko Nchini Gabon.
Timu zilizofuzu mpaka sasa. #AFCON2017
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia
Facebook
,
Twitter na
Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment