Huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo
kikitangaza kuhairisha Maandamano ya nchi nzima yaliyopewa jina la
UKUTA, wakidai kuwa viongozi wa Dini wamewaomba wasitishe ili waweze
kutafuta suluhu kwa kuzungumza na Rais Magufuli.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ameeleza
kuwa licha ya kuhairisha kwa maandamano ya UKUTA kwa muda wa mwezi
mmoja, kumefanyika uonevu kwa serikali kuvifungia vyombo vya habari vya
Radio 5, Magic FM na Gazeti la Mseto kwa kile anachodai kuwa vimekuwa
zikiripoti habari za UKUTA nidyo maana vimefungiwa.
Hivyo ameeleani vikali kitendo hicho na
kueleza kuwa hiyo ni dhahiri kuwa nchi hii haifuati misingi ya haki na
sheria, huku akifafanua kuwa imefikia hatua vyombo vya usalama
vinaingilia muhimili wa vyomba vya habari na kuwataka kuandika vichwa
vya habari wanavyoona vinafaa.
Ambapo amesisitiza kuwa wataendelea
kupambana ilikufanikisha kuwa haki inapatikana na kila Mtanzania anaishi
kwa amani kwenye Taifa lake.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment