Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu.
Hayo
yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Nchini (TCRA) Eng. James Kilaba katika mkutano wa kimataifa
wa wadau wa mawasiliano ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la
Mawasiliano (ITU) kwa kushirikiana na TCRA pamoja na Benki Kuu ya
Tanzania (BOT).
“Huduma
za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini Tanzania imepiga hatua kubwa
,ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia
ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa
kutumia mitandao ya simu,” alisema.
Kuhusu
mkutano huo wa kimataifa ulioshirikisha washiriki zaidi ya 150 kutoka
nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa ITU, alisema umelenga
kujadili namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika
sehemu ambazo hazifikiwi na huduma hiyo.
“Mkutano
huu unasimamiwa na shirika la mawasiliano duniani ITC ambao umelenga
kujadili namna ya kutumia mitandao ya simu kupeleka huduma za kifedha
katika maeneo yasiyofikiwa na huduma za kifedha hasa ambako hakuna
mabenki. Mkutano huu nchi imeamua kuuanda kwa ushirikiano wa TCRA na
BOT, ” alisema.
Naye
Gavana Mkuu wa BOT Profesa Benno Ndulu alisema hadi mwisho wa mwezi
Julai mwaka huu takribani watanzania milioni 21.5 nchi nzima wanatumia
huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu.
“Hadi
kufikia Julai, 2016 watanzania 21.5 milioni wanatumia mitandao ya simu
walau mara 1 kwa mwezi idadi hii ni kubwa na kwamba inaonesha sekta hii
inakua kwa kasi,” alisema.
Profesa Ndulu alisema kuwa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu imesaidia kukuza uchumi wa nchi.
“Malipo
ya fedha kwa njia ya simu yanasaidia kupunguza gharama hivyo na kuwa
kichochea cha maendeleo, sasa hivi wafanyakazi, wakulima, wanaotumia
huduma za bima, wanaonunua bidhaa hulipa kwa Kutumia simu za mkononi
hususani kwamba muda ndio muhimu,” alisema.
Aliongeza kuwa “Mitandao
ya simu haiathiri huduma za kibenki, na benki wamechangamkia kutumia
mitandao kufikia wateja wao, hutumia mawakala kufungulia account,
mitandao hii husaidia benki kufikia wateja kote nchini, woga huo
umepungua kwa sasa,”
0 comments:
Post a Comment