Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla ameagiza waajili wote nchini kutoajili wataalamu
wasio sajiliwa na wataalamu wa Baraza la Maabara za Afya nchini ili
kuepuka kuajili wataalam hewa.
Dk. Kigwangalla ameyasema hayo jana
wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wataalamu wa Huduma za Maabara za Afya
tukio lililofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Naibu Waziri alikuwa
mgeni rasmi huku akitoa vyeti kwa wajumbe wa Baraza hilo waliomaliza
muda wao pamoja na wajumbe wapya.
Akipongeza Baraza hilo la Maabara, alisema
kuwa licha ya kuwa ni la siku nyingi, amelitaka kuhakikisha
wanashirikiana na Mamlaka zingine husika kusimamia ubora wa wataalamu
kusimamia vyuo husika katika kuwapata wataalam hao.
Pia aliwataka
wataalamu wa Maabara waliosajiliwa kwa sheria ya 12 ya 1997, wajisajili
tena upya kwa sheria mpya ya namba 22 ya mwaka 2007 kama ilivyoelekezwa
ili wapate vyeti vipya.
Mwisho aliwaagiza
wataalamu woye wa maabara waliosajiliwa wahakikishe wanalipia ada ya
usajili kila mwaka ili kuendelea kupata kibali cha kuendelea kutoa
huduma cha maabara kwa mwaka mzima ili baraza hilo liweze kujiendesha.
“Ili
muwe wataalam, lazima muwe na chombo kama hichi. Hivyo katika msingi
huo nyie wataalum wenyewe mutakiwa kujiongeza katika kuhakikisha
munapata fedha kwa kuchangia/kuchangishana muweze kujindesha kama
yalivyo mabaraza mengine” alisema Dk.Kigwangalla.
Baraza
la Wataalamu wa Maabara za Afya, ni chombo cha kisheria kilichowekwa na
Serikali ili kuwatambua na kuwasajili Wataalamu wa Maabara za Afya ya
Binadamu, kusimamia ubora wa utoaji wa huduma za uchunguzi wa magonjwa
ya binadamu, kuchukua hatua za kisheria kwa wakiukaji wa sheria, na
kushauri Serikali katika kuboresha huduma za maabara kwa wagonjwa.
0 comments:
Post a Comment