Benki
ya Posta Tanzania (TPB) imetoa mchango wa madawati na viti 50 vyote
vikiwa na thamani ya shilingi Milioni Nane kwa Shule ya Sekondari ya
Ikoma, iliyopo Wilayani Serengeti Mkoani Mara.
Mchango
huo wa madawati ulikabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin
Babu na Afisa Mtendaji Mkuu wa (TPB) Sabasaba Moshingi, kwenye hafla
fupi iliyofanyika shuleni hapo.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Sabasaba Moshingi alisema kuwa benki yake
imeamua kutoa viti pamoja na madawati hayo ili kuhakikisha kuwa
wanafunzi wote watakaoanza kutumia shule hiyo hapo mwakani watakaa
kwenye mazingira mazuri yanayofaa.
Pia
alitoa pongezi nyingi kwa uongozi wa Kijiji hicho cha Ikoma kwa bidii
zao zilizohakikisha kuwa wanakamilisha ujenzi wa madarasa pamoja na
maabara, tayari kwa kupokea wanafunzi mwaka ujao.
Aliahidi
kuendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi huo ili kuweza kukabiliana na
changamoto nyingine kama vile uhaba wa nyumba za waalimu na mabweni
zinazoendelea kuikabili shule hiyo.
Naye
mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo Mhe. Nurdin Babu aliishukuru Benki ya
Posta kwa msaada huo uliofika wakati muafaka, ambapo shule hiyo
inajiandaa kupokea wanafunzi wapya.
Alisema
kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania mwenye mapenzi mema kuhakikisha kuwa
anatoa kipaumbele kwa sekta ya elimu ili kuwawezesha watoto wetu kupata
elimu kwenye mazingira mazuri. Alitoa wito kwa taasisi nyingine
kuendelea kusaidia sekta ya elimu nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi akimkabidhi moja ya meza Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi akimkabidhi moja ya viti Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu akiongea na akiishukuru benki ya Posta kwa msaada uliotoa.
0 comments:
Post a Comment