Mchezo wa soka ni mchezo wa kiungwana na wa kistaarabu, jambo hili limekuwa likipigiwa sana kelele na shirikisho la mpira wa miguu duniani kuhakikisha mchezo unakuwa salama kuanzia ndani ya uwanja hadi nje ya uwanja.
Kuwa timu tofauti kwenye mechi moja haimaanishi ni uadui, ndiyo maana kuna ndugu na marafiki wanaocheza timu mbili tofauti lakini baada ya dakika 90 kila kitu kinarudi mahala pake na maisha yanaendelea.
Licha ya kuwepo na changamoto kwenye mchezo wa Yanga vs Simba wa October 1 bado kuna wachezaji walionesha uungwana ndani ya dakika 90 huku makocha pia wakiwa mfano katika hilo.
Hizi ni baadhi ya picha ambazo zinaonesha matukio kadhaa ambapo ustaarabu na uungwana ulitumika kuonesha mchezo wa soka si vita wala uadui.
0 comments:
Post a Comment