Wasambazaji wa nguzo katika kiwanda cha
SAO Hill cha wilayani Mufindi kinachoendeshwa na kampuni ya Green
Resources Ltd. wameilalamikia kampuni hiyo kushindwa kuwalipa fedha za
mauzo ya nguzo kwa wakati hali inayosababisha wasambazaji hao kushindwa
kuendesha biashara zao huku mali zao zikiwa hatarini kufilisiwa na
taasisi za mikopo.
Baadhi ya wasambazaji waliokutwa
kiwandani hapo wakisubiri kuonana na uongozi wa kampuni ya SAO Hill
Industries inayomilikiwa na kampuni ya Green Resources wamesema
makubaliano waliyoingia na kampuni hiyo ni kulipwa fedha zao mara
wanapofikisha magogo kiwandani hapo jambo ambalo lilitekelezwa mpaka
mwezi Septemba mwaka huu.
Aidha wafanyabiashara hao
wamelalamikia makato ya asilimia tano kwaajili ya ushuru wa halmashauri
wanayokatwa kwenye malipo yao na kampuni ya SAO Hill Industries licha ya
wao kuwa wamekwishalipia na kuongeza kuwa wanapojaribu kuonana na
uongozi wa kampuni hiyo wamekuwa wakizuiliwa getini hivyo kushindwa
kujua hatma ya malipo yao.
Meneja mkuu wa kapuni ya SAO Hill
Industries Bw Beatus Bahati amekiri kampuni hiyo kudaiwa na wasambazi
hao wa nguzo na kueleza kuwa kampuni imeshindwa kuwalipa kwa wakati
kutokana na wateja wake wakubwa wakiwemo shirika la umeme nchini TANESCO
kuchelewesha malipo yao huku mauzo ya mbao na nguzo yakiwa yameshuka
kwa kiasi kikubwa.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
WAFANYABIASHARA NGUZO ZA UMEME WALIA KUTOLIPWA STAHIKI ZAO
Reviewed by Newspointtz
on
08:50:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment