Mkuu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo
ameiomba Serikali kufanya tathmini ya haraka kubaini upungufu wa chakula
nchini uliosababishwa na ukame wa muda mrefu.
Akizungumza
wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Meru, Elias
Nassari katika Usharika wa Usa River, Wilaya ya Arumeru alisema kuwa
Serikali haitakiwi kungoja hadi watu wafe ndiyo waanze kutafuta
chakula.
Dk
Shoo ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Mwenyekiti wa Baraza la
Maaskofu Katoliki (TEC), Tarcisius Ngalalekumtwa kuwaandikia maaskofu
wote wa kanisa hilo kuwataka waumini wao wafanye maombi, hija, mfungo
kwa lengo la kukabiliana na ukame unaolikabili taifa.
Vilevile,
hivi karibuni Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) lilitoa wito kama
huo kwa waumini wake, huku Serikali ikisisitiza kuwa hakuna njaa nchini
na kuwa haitatoa chakula cha msaada.
Askofu
Shoo aliitaka Serikali iwajibike kufanya tathimini za haraka ili
kubaini watu walioathirika na njaa pamoja na kujua idadi kamili ya
familia pamoja na kaya zitakazoathirika na njaa ili kupata kiwango
sahihi cha misaada ya chakula kitakachoitajika nchini.
“Mikoa ya Kaskazini njaa ni tishio, kuna familia tunajua hazina chakula na tumeanza kutoa misaada,” alisema Dk Shoo.
Hata
hivyo, alisema kama kanisa wataendelea kufanya maombi ya mvua lakini
ameitaka Serikali kuchukulia suala la ukame kwa umakini kwa kuwa
viashiria vya kuwepo na njaa nchini vimeanza kuonekana.
Awali,
akizungumza kwenye ibada hiyo, Dk Shoo aliwataka viongozi wa dini na
taasisi mbalimbali kutokuwa na kiburi pindi wanapopata madaraka badala
yake wawatumikie waumini na wananchi kama walivyopewa dhamana hiyo.
“Kiburi
ni tishio sana hasa pale kiongozi atakapoonyesha, tuombe Mungu sana
tabia hiyo isiwepo kwa viongozi wetu wa makanisa na taasisi mbalimbali
nchini,” alisema Dk Shoo katika ibada iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa.
Viongozi
waliokuwapo ni Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba,
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Meya wa Jiji la Arusha, Calist
Lazaro na wabunge Lazaro Nyalandu (Singida Kaskazini) na Joshua Nassari
wa Arumeru Mashariki.
Alipopata fursa ya kuzungumza, Gambo ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli aliyataka makanisa yote nchini kuwashauri wananchi wake kuweka akiba ya chakula ili kukabiliana na ukame uliopo kwa sasa.
Alipopata fursa ya kuzungumza, Gambo ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli aliyataka makanisa yote nchini kuwashauri wananchi wake kuweka akiba ya chakula ili kukabiliana na ukame uliopo kwa sasa.
Pia
aliwataka wawashauri wananchi kupanda mazao ambayo yanastahimili ukame
ili kuepusha tishio la njaa linalotokana na ukame na wakulima ambao
wanasafirisha mazao nje ya nchi kuacha mara moja.
Kuhusu
migogoro ya ardhi inayoendelea nchini, Gambo alizitaka taasisi za
kidini kuyalinda maeneo yao akisema kumezuka mtindo kwa baadhi ya watu
kuingilia maeneo ya taasisi hizo.
Akitoa
shukrani baada ya kusimikwa, Askofu Nassari aliwataka viongozi
mbalimbali wa kidini kuhakikisha malengo ya kanisa yanatimia.
Pia alisema atashirikiana na viongozi wa kisiasa na kijamii kuhakikisha changamoto mbalimbali za kijamii zinatatulika.
Chadema kugawa chakula
Wakati huohuo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa alisema kwa kuwa Serikali haina utaratibu wa kutafuta ufumbuzi wa tatizo la chakula nchini, chama chake kitaandaa utaratibu wa kuhakikisha chakula kinapatikana.
Wakati huohuo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa alisema kwa kuwa Serikali haina utaratibu wa kutafuta ufumbuzi wa tatizo la chakula nchini, chama chake kitaandaa utaratibu wa kuhakikisha chakula kinapatikana.
Alisema
Chadema ina uwezo wa kuomba chakula hata kutoka nje ya nchi ili
kuhakikisha hakuna mwananchi atakayepoteza maisha kwa tatizo hilo.
Alisema hayo katika hotuba yake aliyoitoa mjini Bukoba kwa viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya matawi hadi wilaya.
Alisema
jambo kubwa linalomvutia kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump ni
uwezekano wa kuwabana viongozi wa Afrika wanaochezea demokrasia.
“Nawaambia
viongozi wa dunia wajue demokrasia ni lazima ipewe nafasi yake katika
nchi za Kiafrika na si kuacha iendelee kuchezewa,” alisema Lowassa aliyegombea urais akaibuka wa pili nyuma ya Rais Magufuli mwaka jana.
Pia,
Lowassa aliwaeleza kuwa haina maana kusema kuna amani na utulivu
wakati hakuna demokrasia na kudai kinachoendelea nchini kwa sasa ni
kuwajenga hofu wananchi.
“Kinachofanyika hivi sasa ni kujenga watu hofu na kupandikiza chuki, kufanya hivyo ni kujenga mazingira ya udikteta,” alifafanua Lowassa.
“Kinachofanyika hivi sasa ni kujenga watu hofu na kupandikiza chuki, kufanya hivyo ni kujenga mazingira ya udikteta,” alifafanua Lowassa.
Pia, alikosoa matamko yanayotolewa na Rais Magufuli akisema haoni kama yanazingatia ushauri wa wataalamu wengine.
Alidai kuwa hakuna sababu ya kujivunia ununuzi wa ndege mpya wakati kuna matatizo mengine sugu yanayowatesa Watanzania.
Alidai kuwa hakuna sababu ya kujivunia ununuzi wa ndege mpya wakati kuna matatizo mengine sugu yanayowatesa Watanzania.
“Rais
anatakiwa kutumia wataalamu kabla ya kutoa misimamo yake sioni sehemu
anaposhauriwa na mawaziri, sioni cabinet inayomshauri kuhusu suala la
njaa,” alisema Lowassa aliyewahi kuwa waziri mkuu.
Alisema
ununuzi wa ndege ungesubiri na badala yake fedha hizo kutatua tatizo la
maji linalowakabili wananchi wengi huku akirejea alivyoshughulikia
tatizo hilo akiwa Waziri wa Maji.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya chama hicho Profesa Mwesiga Baregu alisema nguvu kubwa
inayotumika kubana vyama vya upinzani inatia shaka na kujenga hofu kwa
wananchi.
Alitoa
mfano wa nguvu kubwa iliyotumika kuzuia mikutano ya Ukuta kuwa ni
dalili za kutojiamini kwa Serikali kiasi cha kuvuruga utaratibu wa
kidemokrasia.
0 comments:
Post a Comment