Mfuko
wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika kuhakikisha inatatua
changamoto ya ukosefu wa ajira hasa kwa vijana umeamua kuachana na
uwekezaji wa majengo makubwa na badala yake imeanza kuelekeza nguvu
katika kufufua viwanda.
NSSF
imeazimia kuunga mkono malengo ya Rais John Magufuli ya kukuza uchumi
kwa kufufua viwanda na kwa kuanzia mfuko huo umeamua kufufua viwanda vya
usagishaji vilivyokuwa katika mikoa ya Iringa, Mwanza, Dodoma na
Morogoro.
Hivi karibuni, Rais Magufuli aliagiza mifuko hiyo kuachana na ujenzi wa majengo badala yake ikijike katika ujenzi wa viwanda.
Kaimu
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Bathon Mmuni alisema hayo mjini
Morogoro katika mkutano uliowakutanisha wadau wa mfuko huo kutoka
taasisi za Serikali na binafsi ili kujadili masuala mbalimbali kuhusiana
na mfuko huo.
“Lazima
fedha wanazochanga wanachama zizalishe haziwezi kukaa tu, uwekezaji ni
moja ya faida kwa mwanachama wetu, hivyo lazima tubadilishe uwekezaji
ili kupata faida,” alisema.
Mmuni
alisema kwa muda mrefu nchi imekuwa na changamoto ya ajira hasa kwa
vijana, hivyo wameamua kufanya uwekezaji upande mwingine ikiwa katika
kufufua na kujenga viwanda.
Alisema ili kumsaidia Rais Magufuli katika kukuza uchumi, mbali na usagishaji wanaelekeza nguvu katika viwanda vya sukari.
Alisema
mfuko huo pia unalenga kuwawezesha Watanzania kupata ajira, hususani
kwa vijana na kwa kuanzia shirika litaanza na ujenzi wa kiwanda cha
sukari katika eneo la Mkulazi kwa kushirikiana na Mfuko wa Pensheni wa
PPF kupitia kampuni tanzu ya Mkulazi Holding.
Kaimu
Mkurugenzi wa Fedha wa NSSF, Tikyeba Alphonce alitaja baadhi ya
changamoto zinazoukabili mfuko huo kuwa ni baadhi ya waajiri kuchelewa
kuwasilisha fedha za wanachama.
0 comments:
Post a Comment