Kila ifikapo tarehe 22 mwezi wa Nne kila
mwaka duniani huadhimishwa siku ya utunzaji wa mazingira, vijana washauriwa
kutumia ujuzi walionao kujitolea kuyatunza na kuyalinda mazingira kwa manufaa
ya vizazi vijavyo.
Haya yameelezwa na muwakilishi wa Tanzania
kutoka taasisi ya World merit (country representative), Rose Mbaga katika
ukumbi wa Freedom square uliyopo chuo kikuu cha SUA fakati ya science Mazimbu,
Morogoro.
Rose akazungumzia makutano hayo na dhumuni
la kuadhimiza siku hiyo ni kuwahamasisha vijana kujitambua nafasi kubwa
waliyonayo katika kusimamia na kuyatunza mazingira wakiwa ni nguvu kazi ya
taifa.
“kulingana na wingi wa nguvu kazi ya vijana
nchini hata duniani hivyo tukaona ni fursa sasa kwa wingi huu wa vijana
kuwahamasisha na kuwafanya kuwa kipaumbele katika kuyatunza na kulinda
mazingira ili hata wanyama na wadudu watambue uwepo na nguvu za vijana” alieleza
Rose.
Amesema kwa kushirikiana na mashirika kama
Raleigh Tanzania, Global peace foundation, Economic diplomacy wameadhimia
kuwafikia vijana kuwapatia elimu ya utunzaji mazingira kwakuwa nafasi ya
utunzaji tegemezi ni vijana wenyewe na kuiita siku hii ni Earthday Tanzania.
Kwa upande wake muwakilishi wa Global peace foundation
Tanzania, Kamara Dickson alisema siku ya maadhimisho hayo ni muda muafaka kwa
jamii kujitahimini katika matumizi ya rasilimali kwa kizazi cha sasa.
“Earth
day Tanzania ni wakati mzuri kwa watu kutambua kuwa wao ndio chanzo tegemezi
kwa kulinda mazingira kwaajili ya jamii ijayo kunufaika na utunzaji wa sasa,
pasipokuwa na usimamizi na utunzaji mzuri hivi sasa hakika vizazi vyetu vijavyo
havitoweza kushi kwa muda mrefu” alifafanua Kamara.
Katika kongamano hilo mbali na kuadhimisha
siku ya utunzaji wa mazingira duniani vijana wamehaswa kuchangamkia fursa mbali
mbali zitolewazo na taasisi za hapa nchini.
Baadhi ya washiriki katika maadhimisho yahayo
nao walifurahia nafasi ya vijana kuwa kipaumbele kila sekta pia kutoa pongezi
za dhati kwa waandaaji kuwakumbusha vijana nafasi waliyonayo katika jamii.
“kupitia mafunzo ya leo
nimejifunza vitu vingi mbali na kijana tambua nafasi yao katika kutunza
mazingira pia tunapaswa kudhubutu, kwani vijana wengi wamekuwa na maono mengi
ila kudhubutu kuyatekeleza mawazo yao imekuwa ni ngumu” alisema mmoja wa
waudhuriaji, Theresia Chua.
0 comments:
Post a Comment