WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea Taarifa ya Kamati Shirikishi ya Mkuu wa
Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya
ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo mkoani Arusha, ambapo atatoa
maelekezo baada ya kuisoma.
Alipokea
taarifa hiyo juzi katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa Spika,
Bungeni mjini Dodoma. Waziri Mkuu aliiunda kamati hiyo, Desemba mwaka
jana mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi mkoani Arusha.
Kiini
cha mgogoro huo ni eneo la pori tengefu la Loliondo ambalo linagombewa
na wawekezaji, wakulima, wawindaji kwa sababu ni mapitio ya wanyama,
chanzo cha maji, mazalia ya wanyama, malisho ya mifugo na makazi.
Kikao
hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Tate
William Ole-Nasha, viongozi wa mkoa wa Arusha na wataalamu kutoka Wizara
ya Maliasili na Utalii. Wengine ni Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid
Taka, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa wa Arusha na wilaya ya
Ngorongoro, wawakilishi wa wananchi, wawekezaji na asasi za kiraia ambao
wote walishiriki katika uandaaji wa taarifa hiyo.
Waziri
Mkuu alisema lengo la kamati hiyo ni kutaka kupata muafaka wa matumizi
ya rasilimali zilizoko katika eneo hilo ili kila upande uweze kutekeleza
majukumu yake bila ya kuathiri mwingine na kuwezesha wananchi wote
kunufaika na rasilimali zilizoko katika eneo hilo.
“Serikali
inataka watu wote tuwe kitu kimoja katika kutunza maeneo yetu, lakini
pia shughuli za wananchi nazo ziweze kuendelea ili Watanzania wote
tuweze kunufaika na rasilimali zilizoko kwenye maeneo yetu,” alisema.
0 comments:
Post a Comment