NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Mahakama Singida yawahukumu majangili saba kwenda jela miaka 140 na faini ya Bilioni 1.9

newspointtz.blog

Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Singida, imewahukumu majangili saba adhabu ya kutumikia jela ya miaka 140 na kulipa faini ya zaidi ya shilingi 1.9 bilioni baada ya kuwatia hatiani kwa kwa makosa 12  likiemo la kumiliki bunduki ya kijeshi SMG waliyokuwa wanaitumia kuulia Tembo.

Baadhi ya makosa mengine ni kuunda umoja /ushirikiano wa kufanya uhalifu wa  kuuawa  wanyapori wakiwemo Tembo, kufanya biashara haramu ya kuuza nyara za serikali na kumiliki meno ya Tembo bila kwa na kibali.

Washitakiwa hao ambao kesi yao ilipewa namba 5/2015, ni Yusuph Masala Jidavi (39) mkulima kijiji cha Yongo Manda mkoani Katavi, Elias John  Sprian (30) mkazi wa Kijiji cha Ng’ambe mkoani Tabora na Salum Mohammed Ngasa (31) mkazi wa kijiji cha Imalampaka Sasilo wilaya ya Manyoni.

Wengine ni Yona  Stanley @Yohana (26) mkazi wa kijiji cha Mbwasa Sasilo wilaya ya Manyoni, Ramadhani Salum Hatibu (33) mkulima kijiji cha Mgulu wa Ng’ambe wilaya ya Manyoni,Kulwa Saidi Salum (28) mkulima kijiji cha Sikonge mkoani Tabora na Buhoro Salehe Lubaha Yakonie (37)@  Buhoro  mkazi wa Kambi ya Wakimbizi Katumba mkoani Tabora.

Mwendesha mashtaka na mwanasheria wa serikali Pretrida Mutta, alidai mbele ya Hakimu mfawidhi mwandamizi na mahakama hiyo, Joyce Minde, kuwa kati ya Agosti mwaka 2013 na Julai nane mwaka 2014, washitakiwa kwa pamoja walikamatwa wakimiliki vipande 28 vya meno ya Tembo vyenye thamani zaidi ya shilling 34.1 milioni.

Mutta alisema pia washitakiwa hao walikamatwa wakimiliki kinyume na sheria ‘Elephant tufts’ sita zenye thamani ya shilingi 192 milioni, kipande cha ngozi ya Simba chenye thamani ya zaidi ya shilingi 7.8 milioni na ngozi ya kudu ya shilingi 3.5 milioni.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu, Mwanasheria wa serikali Mutta, aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa washitakiwa, ili iwe fundisho kwao na kuogofya watu wengine wanaotarajia kujihusisha biashara haramu ya kuuza nyara za serikali.

Kwa upande wa washitakiwa ambao wakili wao na kujitegemea Josephat Wawa ambaye hakuwepo Mahakamani, washitakiwa kila mmoja kwa wakati wake, aliiomba mahaka hiyo impe adhabu nafuu kwa madai mbalimbali likiwemola kutegemewa na familia.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Minde, alisema kuwa upande wa mashitaka umethibitisha bila kuacha chembe chembe ya shaka kwa hali hiyo washitakiwa wana hatia kama walivyoshitakiwa.
“Kila mshitakiwa atatumikia jela miaka 20 na kulipa faini ya zaidi ya shilingi 274.2 milioni adhabu hizi ni fundisho kwenu na pia kuwaogofya watu wengine wanaotarajia kutenda makosa ya aina hii”,alisema Hakimu Minde.

chanzo>Moblog
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment