NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

FID Q: TUSIMDHARAU CHID BEENZ

SHARE

Rapa mahiri nchini Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q amefungukia suala la rapa anayefananishwa nae kimichano maarufu kama Stamina kukanusha kujiita Chid Beenz.

Akizungumzia suala hilo katika mahojiano yake na kipindi cha Planet Bongo ya East Afrika Radio rapa huyo amesema hashangai watu kumfananisha na Stamina kimashairi na kuongeza kuwa kila mtu anatambua kuwa Stamina amewahi kutangaza kufuata nyayo zake na amekuwa akifanya hivyo kwenye nyimbo zake.

Akizungumzia suala la Chid Beenz rapa huyo ameeleza kuwa bado anaamini uwezo wa Chid Beenz hivyo hakuna sababu ya kumdharau kutokana na kupotea kwake kwenye game, huku akieleza kwa jinsi anavyo amini uwezo wa Chid Beenz hakuna kinacho mshinda kwenye staili ya michano

 

chanzo>mtembezi


Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment