Juanfran alifunga penati ya ushindi kuiwezesha Atletico Madrid kuiondosha PSV Eindhoven kwenye michuano ya Ulaya kwa mikwaju 8-7 na kufuzu hatua ya robo fainali.
Timu hizo zilishindwa kutambiana katiaka dakika za kawaida 210, ikiwa ni mara ya kwanza kwenye hatua ya mtoano ya Champions League timu kutoka sare ya bila kufngana kwa michezo yote miwili.
Katika kiwango bora cha upigaji penati, zilishuhudiwa penati 14 zikizama kambani lakini Luciano Narsingh ambaye aliingia dakika za mwisho kuchukua nafasi ya Luuk de Jong, penati yake iligonga mwamba na kushuhudia timu yke kutoka Uholanzi ikiyaaga mashindano.
Rekodi muhimu zilizowekwa kwenye mchezo huo
- Atletico Madrid ilifanya attempt 26 (pamoja na mashuti yaliyokuwa- blocked) kwenye mchezo huo lakini hawakufanikiwa kufunga goli, ikiwa ni attempt nyingi kufanywa kwenye michuano ya Champions League tangu Sporting Braga walipofanya hivyo dhidi ya Cluj September 2012 (mashuti 38 bila goli)
- Jan Oblak ameendelea kuweka rekodi ya kutoruhusu bao langoni kwa Atletico kwenye mashindano yote msimu huu, mechi nyingi zaidi ya golikipa yeyote kutoka ligi tano kubwa za Ulaya msimu huu
- Atletico Madrid wamefikisha mchezo wa 13 bila kuruhusu bao kati ya michezo 17 ya Champions League
- Hatua ya matuta ilimalizika 8-7, penati nyingi kuwahi kufungwa kwenye historia ya michuano ya Champions League/European Cup
0 comments:
Post a Comment