Seneta wa Florida Marco Rubio
amesitisha kampeni yake ya kusaka tiketi ya kuwania urais kupitia chama
cha Republican Marekani baada ya kushindwa nyumbani katika mchujo wa
chama hicho.
“Hali kwamba nimefika mbali hivi ni ishara ya jinsi Amerika ilivyo nchi ya kipekee,” alisema akitangaza kujiondoa.Mgombea anayeongoza katika chama hicho, mfanyabiashara Donald Trump ambaye amekuwa akishambulia sana Marco Rubio siku za hivi karibuni, amempongeza kwa kuendesha “kampeni kali”.
Trump, akihutubia mkutano katika hoteli ya Mar-a-Lago, amesema Rubio ni mgombea “mkali, mwerevu” na mwenye matumaini makubwa siku za usoni.
Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York ameshinda katika majimbo ya North Carolina, Illinois na Florida katika mchujo wa chama cha Republican Jumanne.
John Kasich ameshinda jimbo lake la kwanza kabisa, kwa kupata ushindi jimbo lake la Ohio.
Ted Cruz, anayemfuata Trump hajashinda jimbo lolote kati ya majimbo yaliyoshiriki mchujo Jumanne.
chanzo>BBC
0 comments:
Post a Comment