Nikk Wa Pili ajibu kwanini amewadhihaki Arsenal kwenye instagram
Kama wewe unamfuatilia Nikk wa Pili kwenye instagram basi utakua umeshaona post ambayo inaonyesha Wenger anasali akiomba kutokana na mechi iliyopo mbele yake.
Baadhi ya mashabiki kutokana na ushabiki wao wameona kama wamedhihakiwa na timu yao lakini Nikki ametoa maelezo juu ya post ile.
Swali : Kwanini umeweka ile picha kwenye instagram
Jibu : Kulingana na nature ya mechi na Arsenal yenyewe, Arsenal ni wazuri wakishambuli wakiwa wanapanda wote. Sasa kama uliangalia mechi ya Emirates ni kwamba Arsenal walifungwa tu pale ambapo back 4 yao ilipanda. Maana yake ni kwamba ukiwaacha Messi, Neymar, Suarez peke yao ikipigwa counter attack ni maafa kwa upande wa Arsenal. The only way ambayo Arsenal wanaweza kubaki salama ni kuhakikisha back four yao inabaki sehemu husika.
Sasa Arsenal wakicheza hivyo ina maanisha kwamba uwezo wao kushambulia utakua mdogo sana na Arsenal leo wanatakiwa washambulie ili wapate goli.
Sasa kitendo cha Arsenal kwenda mbele kushambulia leo ni hatari zaidi kwao. Ushaona hapo technically huu ni mchezo mgumu sana kwa Arsenal kama wakishambulia au hata wasiposhambulia matokeo yatakua mabaya kwao.
Swali : Rafiki yako G Nako ni shabiki wa Arsenal, hivi huwa ana bet
Jibu : G Nako nishamkataza kushangilia timu mbovu lakini yeye bado anaendelea inaonyesha jinsi gani amezoea maumivu. Kwenye swala la ku-bet G Nako sio mtu wa ku-bet, yeye anafuatilia tu maumivu ya Arsenal kama mashabiki wengine.
Swali : Kwa watu ambao wanaotaka ku-bet leo unawashauri nini?
Jibu : Nadhani jibu tayari wanalijua, hii mechi iliisha tangu kwenye mechi ya kwanza. Kila mtu anamjua mshindi ni nani. Kama unataka kula weka Barcelona.
0 comments:
Post a Comment