MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea na Manase Mjema, Diwani wa Kimanga wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi na kusomewa shitaka la kudhuru mwili ambapo wote wawili wamekana shitaka hilo.
Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kumshambulia Terresia Mmbaando, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mkutano wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam tarehe 27 Februari 2016.
Kubenea anatajwa kuwa ni mtuhumiwa namba sita ambapo Manase akiwa mtuhumiwa namba nne.
Mmbando
alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es
Salaam uliofanyika kwenye Ukumbu wa Kareem Jee na baadaye kuahirishwa
hatua ambayo iliibua malumbano.
Mbele
ya Cyprian Mheka, Hakimi Mkazi Kisutu washitakiwa hao walikana kosa
hilo ambapo hakimu alighairisha kesi hiyo mpaka tarehe 16 Machi mwaka
huu.
Hata hivyo, Hakimu Mkeha aliwataka watuhumiwa hao kujidhamini wenyewe kwa dhamana ya Sh. 2,000,000 sharti ambalo wamelitekeleza.
Jana
asubuhi kwenye mahakama hiyo Kubenea akihudhuria kesi yake dhidi ya
Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, alikamatwa na Jeshi la Polisi
na kuwekwa chini ya ulinzi.
Kubenea
na Manase wameunganishwa kwenye kesi hiyo ambapo watuhumiwa
waliofikishwa mahakamni awali ni Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Mwita
Waitara, Mbunge wa Ukonga na madiwani wawili jumla yao ikiwa ni
watuhumiwa sita.
chanzo>mpekuzi
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook
, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment