Chama cha Wanasheria Wanawake nchini (TAWLA) kimetoa mafunzo kwa waandishi wa habari yanayolenga kujenga uelewa kwa waandishi wa habari kuhusiana na masuala ya haki ya afya ya uzazi, changamoto wanazokutana nazo na namna ambavyo matumizi ya sheria za kimataifa zitaweza kupunguza chanagamoto hizo.
1
Afisa Uchechemuzi wa Shirika la Wanasheria wanawake la TAWLA Bi. Sime Bateyunga akifungua mafunzo kwa wanahabari hawapo pichani yanayolenga kujenga uelewa kwa waandishi wa habari kuhusiana na masuala ya haki ya afya ya uzazi, changamoto wanazokutana nazo na namna ambavyo matumizi ya sheria za kimataifa kama Maputo Protocal yataweza kupunguza changamoto hizo, Semina hiyo ya siku mbili ilikuwa ikifanyika Luther House Azania Front jijini Dar es salaam na imemalizika leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Wanahabari wakimsikiliza Afisa Uchechemuzi wa Shirika la Wanasheria wanawake la TAWLA Bi. Sime Bateyunga wakati akifungua semina hiyo jana.
4
Dk. Ali Said kutoka muhimbi akiwasilisha mada katika mafunzo hayo kuhusu utoaji mimba usio salama na madhara yake.
5
Afisa habari na mawasiliano TAWLA, Goodness Mrema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo leo.
6
Afisa Mipango wa TAWLA, Bi. Sara Kinyaga kulia akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuendesha mafunzo hayo kwa waandishi wa habari leo.
7
Maofisa wa TAWLA pamoja na waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo leo jijini Dar es salaam.