NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Uchaguzi wa Marudio Zanzibar Unaendelea Kwa AMANI na UTULIVU.......Wananchi Wameitikia na Ulinzi Umeimarishwa

Wananchi wa Zanzibar leo wanapiga kura katika uchanguzi wa marudio baada ya kufutwa kwa uchanguzi uliofanyika October 25,2025 kutokana na kasoro zilizojitokeza.

Katika baadhi ya vituo wananchi wamejitokeza na zoezi linaendelea vizuri huku hali ya usalama ikiwa imeimarishwa.

Katika kituo cha shule ya sekondari Muembeladu ambayo ina vituo sita,vituo vitano vinawatu 350 na kituo kimoja kina watu 91. Akizungumza na wanahabari, msimamizi wa kituo hicho amesema zoezi la upigaji kura linaendelea vizuri katika jimbo la Jangombe .

Kwa upande wa kituo cha skuli ya Muembeshauri nako hali ni shwari na zoezi linaendelea vizuri ambapo katika skul hiyo vituo 11 vinatumika watu kupiga kura.
Katika Jimbo la kikwajuni, zoezi  linaendelea vizuri huku mwitikio wa watu ukiwa ni mkubwa.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wamesema zoezi hilo limekua rahisi na la  amani tofauti na taarifa zilivyokua zinasambazwa.

Mkazi wa Muembeshauri aliyejitambulisha kwa jina la Hamidu Salum Haji ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwani zoezi la kupiga kura linaendelea kwa amani na utulivu.

Ndugu zangu tusikubali kugombanishwa na watu ambao hawaitakii mema Zanzibar tusimame pamoja katika kutetea nchi yetu” amesema Haji
 
Wakati zoezi hilo linaendelea maduka mengi yamefunguliwa na wafanyabiashara wanaendelea na kazi kama kawaida.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment