Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema, Yanga Makaga (CCM) amemtimua kikaoni Diwani wa kata ya Chifunfu, Robert Madaha (CCM) kwa kosa la utovu wa nidhamu aliouonyesha ndani ya kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo baada ya kumwamuru kutoka nje alipoonyesha kutokuwa na nidhamu ndani ya kikao hicho.

Hatua ya mwenyekiti huyo imekuja  kutokana na madiwani walipokuwa wakichangia hoja mbalimbali za kimaendeleo katika kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo na diwani huyo aliyetimuliwa kuharibu michango mbalimbali inayotolewa na madiwani huku yeye akiwa bado hajaruhusiwa kuchangia chochote kitendo kilichofanya baadhi ya madiwani kuomba mwongozo juu ya swala hilo na ndipo alipoamuliwa kutoka nje naye alikaidi madiwani wenzake walimsihi na kutoka nje huku alikuwa anamgomea mwenyekiti.

 Alisema kuwa kutokana na kifungu cha sheria za kudumu za halmashauri kifungu na 17 kipengele namba a na b kwa mamlaka ya mwenyekiti kupitia baraza hilo diwani huyo hata hudhuria vikao vitatu vya Baraza hilo na hata lipwa chochote hadi atakapo maliza adhabu hiyo aliyopewa kutona na kutokutii mamulaka husika  hiyo hatalipwa na kumwagiza mkurugenzi kutokumlipa .
Daniel Makaka, Sengerema