Wananchi
wa kata ya Nyampulukano, wilayani Sengerema Mkoa Mwanza wanaiomba
serikali ifanye jitihada za haraka kutenga maeneo mengine ya maziko
kutona na maeneo ya sasa kujaa na kuleta adha kwa wananchi wanakwenda
kusitili mwenzao.
Kauli
hiyo ya wananchi imekuja baada ya wananchi wa kata ya nyampulukano
walipokuwa wakichimba kaburi katika makaburi ya waisilamu yaliyoko
kitongoji cha uwanja wandege katika mji wa sengerema baada ya kukutana
na fuvu katika maeneo hayo yanayosababishwa na maeneo hayo kujaa.
Walisema
kuwa katika maisha ya kawaida ya mwanadamu anapofari kiriki ni haki
yake kuzikwa na eneo alilozikwa hatakiwi kubuguziwa lakini hali ya
kubuguziwa imetokea mjini sengeremakutokana na maeneo a maziko kujaa na
wananchi kuutupia lawama uongozi wa halimashauri ya Sengerema
kutokutilia maanani swala la kutenga maeneo ya maziko huku wakijua
maeneo mengine hayana nafasi ya kuzika tena watu waliopoteza uhai.
Baadhi
ya Wananchi waliokuwa wanachimba kaburi na kukutana na fuvu hilo Lenson
Masatu na Kibisa Myoba walisema kuwa nijambo la kushangaza kwa
serikali kutokuona swala hili la kutenga maeneo mengine ndiyo sababu ya
kurudia kuzika mtu mwinge juu ya mwingine kitendo ambacho siyo cha
kiungwana na kinadhalilisha utu wa mwanadamu na kuwaomba walitazame
swala hili kwajicho la huruma kwa wanandamu
Diwani
wa kata ya Nyampulukano Emanuel Munwazi [Chadema] aliyekuwa
amehudhuria kuchimbaji wa kaburi hiyo na kukutana na fuvu hilo alisema
kuwa amekwisha wasilisha hoja hiyo katika kikao cha Baraza la madiwani
la halimashauri hiyo lililopita juu ya maeno hayo ya maziko kujaa na
maazimio kutotewa lakini cha kushangaza hadi sasa serikali haijaona
umuhimu wa swala hilo ambapo linaweza kusababisha kuleta maafa kwa watu
wakiono kuwa mtu wao alikuwa amezikwa kasha kufukuliwa kuzikwa mwingine.
‘’Ni
jambo la kushangaza na kusikitisha juu ya swala hili kuona serikali
haitilii maanani swala hili huku wawakilishi wa serikali wapo mkurugenzi
yupo, mkuu wa wilaya hupo wameka kimya huku swala kutenga maeneo liko
chini ya uwezo wao wanataka mauwaji yatokee ndipo watenge maeneo hili
ni aibu kwa serikali,” alisema Munwazi.
Kaburi
hilo lilikuwa ni la kumzika Said Bihemo aliyfaliki dunia wilayani
sengerema walimuzika na kishwa fuvu hilo kuliludisha ndani ya kaburi
hilo walichimba baada ya kuzika said kitendo ambacho kilizua vilio na
huzuni kutawala katika makaburi hayo.
Mkurugenzi
wa halimashauri ya Sengerema, Chalya Julias alisema kuwa changamato ya
maeneo la maziko kujamaa yako kila kona ya sengerema hivyo halimashauri
yake iko mbioni kutafuta maeneo ya maziko sehemu nyingine kutokana na
maziko hayo kujaa na kuwaomba wananchi wawe na subila juu ya swala hilo
litatekelezwa. na wakumbuke kuwa kupata maeneo nilazima watu wenyemaeneo
hayo walipwe.
Mwenyekiti
wa halimashauri ya Sengrema, Yanga Makaga alisema kuwa anaona huruma
kuona watu walipoteza uhani wakifukuliwa na kuzikwa mwingine
nakuahidi kulishugulikia swala hilo mapema la kutenga maeno mapya ya
maziko. hivyo wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu.
Na Daniel Makaka
0 comments:
Post a Comment