Upinzani nchini Brazil umefanikiwa
kupata theluthi mbili ya kura zilizokuwa zikitakiwa katika hatua za
kuelekea kupiga kura ya kutokuwa na imani na
Rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff.Maandamano makubwa yanapangwa kufanywa sehemu mbalimbali Brazil, ambako wabunge wanatarajiwa kupiga kura leo, ikiwa wanataka Rais Dilma Rousseff ashtakiwe au la, kwa sababu ya kubadilisha bajeti. Wanaompinga lazima wapate theluthi mbili ya kura zote , kuweza kumshtaki rasmi kiongozi huyo katika baraza la Seneti.
Mamia ya askari polisi wenye silaha wameshika zamu, kujaribu kuzuia makabiliano baina ya waandamanaji wanaopingana, na ambao wamekesha nje katika mji mkuu, Brasilia.
Waandishi wa habari wanasema, kizuizi cha urefu wa mita mbili, kilichowekwa baina ya waandamanaji hao, mahasimu ni ishara ya mgawanyiko mkubwa nchini, baina ya wafuasi na wapinzani wa Rais Rousseff.
Bi Rouissef anakanusha kuwa alibadilisha hesabu za bajeti, kabla ya uchaguzi wa mwaka 2014, ambapo alichaguliwa tena.
Anawashutumu wanasiasa wanaotaka kuitoa madarakani serikali yake iliyochaguliwa na wananchi wa nchi hiyo.
chanzo>bbcswahili
0 comments:
Post a Comment