Kamati maalumu ya uchunguzi iliyoundwa
na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda imefichua madudu na
harufu ya ufisadi katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu
maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya
Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya mji.
Kutokana
na madudu hayo, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha wazi kuwa hataki kufanya
kazi tena na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe na Kaimu
wake, Sarah Yohana na kuwasilisha majina yao kwa mamlaka husika ya
nidhamu kwa hatua zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar
es Salaam jana, alisema hivi karibuni aliunda kamati hiyo maalumu
kufuatilia maeneo hayo muhimu kutokana na malalamiko ya muda mrefu,
ambayo ofisi yake ilikuwa ikipokea kutoka kwa wananchi.
Alisema kwa mujibu wa uchunguzi, kamati
hiyo ilibaini kuwa katika stendi ya mabasi ya Ubungo, kumekuwa na
ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma, ikiwemo kutokuwasilishwa kwa mapato
halisi yanayotokana na makusanyo ya kila siku serikalini.
“Kamati ile imebaini kuwa pale ubungo
kunatumika sheria ndogo mbili za ukusanyaji mapato moja ya mwaka 2004 na
nyingine mwaka 2009 kwa lengo la kunufaisha wachache,” alisema Makonda.
Alifafanua kuwa Sheria Ndogo ya Mwaka
2004 ya ukusanyaji mapato ndani ya kituo hicho, inaonesha kuwa kila basi
linatakiwa kutozwa Sh 4,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh
milioni 42 kutokana na mabasi 350 yanayoegeshwa kituoni hapo.
Hata hivyo, alisema kutokana na
mabadiliko ya tozo, sheria hiyo ilibadilishwa mwaka 2009 na kila basi
likawa linatozwa Sh 8,000 na hivyo makusanyo ya mwezi yakapanda na
kufikia Sh milioni 82 kwa mwezi.
“Lakini cha kushangaza tumebaini kuwa
bado kampuni inayokusanya mapato katika kituo cha Ubungo, inawasilisha
mapato hayo kwa kutumia sheria ya mwaka 2004 yaani Sh milioni 42 badala
ya Sh milioni 82 kwa mwezi…” “…Mbaya zaidi kamati ile katika ukaguzi
wake, ilikuta kampuni ya ukusanyaji mapato hayo stendi ya Ubungo inayo
Sheria ya Mwaka 2009 lakini katika nyaraka za Halmashauri ya Jiji
zinaonesha sheria inayotumika ni ya mwaka 2004,” alisisitiza Makonda.
Alisema katika uchunguzi ilibainika
kuwa kampuni iliyo chini ya Halmashauri ya Jiji inayokusanya mapato hayo
stendi ya Ubungo, ilisaini mkataba wa ukusanyaji mapato hayo kwa mara
ya kwanza Januari 31, 2004 na baadaye ikasaini tena mkataba Januari 30,
mwaka jana.
Kwa mujibu wa Makonda, kwa hali ilivyo
tangu Sheria Ndogo ya Mwaka 2009 ipitishwe, haijawahi kutumika na hivyo
kulisababishia hasara jiji hilo ya Sh bilioni tatu kutokana na mapato
katika stendi hiyo kuendelea kuwasilishwa kwa kutumia sheria ya mwaka
2004.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
MAKONDA:Sihitaji kufanya kazi na mkurugenzi wa Jiji
Reviewed by Newspointtz
on
07:45:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment