Japo nchi ya Marekani imebahatika kuwa na mastaa wengi ambao wanafanya
vizuri kwenye industry ya muziki duniani, lakini kuna ladha za baadhi ya
wasanii ambao imekosekana kwenye nchi hiyo kwa muda mrefu.
Hawa ni baadhi ya mastaa ambao Marekani inatamani kama wangekuwa ni wazawa wa nchi yake.
Hawa ni baadhi ya mastaa ambao Marekani inatamani kama wangekuwa ni wazawa wa nchi yake.
Adele
Jina lake halisi ni Adele Laurie Blue Adkins, alizaliwa mwaka 1988 nhini Uingereza kwenye mji wa London.
Adele amehitimu mafunzo ya muziki kwenye chuo cha Brit School for
Performin Arts and Technology, mwaka 2006. Mwaka 2007 alisaini mkataba
na XL Recording na albumu yake ya kwanza iliofahamika kwa jina la ‘19’
aliyoitoa mwaka 2008.
Mpaka sasa hivi Adele ameshafanikiwa kuachia albumu tatu ‘19’ mwaka
2008, ‘21’ mwaka 2011 na ‘25’ mwaka 2015. Adele ameshafanikiwa kuwa
nominated kwenye tuzo 201 na amefanikiwa kupata tuzo 102 tangu ameingia
kwenye muziki mpaka sasa, zikiwemo tuzo za Grammy, Brit Award, Billboard
Music Award, MTV European Award, American Music Award, European Border
Breakers Award, na nyingine nyingi.
Pia Adele ameshafanikiwa kuweka rekodi kadhaa kwenye Billboard ambazo
hakuna msanii mwengine aliyewahi kuweka, lakini kubwa zaidi ni wimbo
wake wa ‘Hello’ ambao umefanikiwa kuangaliwa mara bilioni mbili kasoro
huku ukifanyiwa Cover na wasanii.
Celine Dion
Celine Dion ni mmoja kati ya wasanii wakubwa na wenye heshima kubwa sana
duniani. Mpaka sasa ana umri wa miaka 48 akiwa ni raia wa nchi ya
Canada.
Celine Dion ni miongoni mwa wasanii matajiri duniani akiwa na utajiri wa
dola milioni 630. Tangu ameanza kuimba akiwa na umri wa miaka 12,
Celine Dion amefanikiwa kupata tuzo 300 kati ya tuzo 400 alizowahi
kushiriki.
Mpaka sasa Celine Dion amefanikiwa kuachia nyimbo zisizopungua 378, kati
ya hizo amefanikiwa kuimba kwa kutumia lugha za nchi tofauti kama vile;
Kiingereza, Kichina, Kifaransa, Kijerumani, Kiitaliano, Kilatini na
Kijapani.
Uwezo wake wa kuimba kwa kupanda hadi kugusa key ya mwisho ndiyo
umewavutia watu wengi na kumfanya kuwa maarufu zaidi duniani. Kutokana
na rekodi aliyoiweka Celine Dion na uwezo aliokuwa nao hakuna msanii
kutoka nchini Marekani ambaye ameweza kuikaribia rekodi yake.
Aubrey Drake Graham
Drake ndiyo jina ambalo linafahamika zaidi kwenye industry ya muziki
duniani. Ni raia wa nchi ya Cannada, lakini ni mwimbaji, mwandishi wa
nyimbo, muandaaji wa muziki na muigizaji pia.
Drake ambaye yupo chini ya lebo ya Young Money Entertainment (YME) aliyosaini mwaka 2009, inayomilikiwa na Lil Wayne.
Nyimbo yake ya ‘Best I Ever Had’ ilifanikiwa kushika namba mbili kwenye
list ya Billboard Hot 100 na albumu yake ya ‘Thank Me Later’ ilifanikiwa
kushika namba moja kwenye Billboard 200.
Drake amefanikiwa kuchukua tuzo za Grammy, tuzo 3 za Juno Awards, tuzo
sita za BET Awards. Kutokana na uwezo wake amefanikiwa kushirikishwa
kwenye nyimbo kibao na wasanii wa kubwa kama Jazz, Kanye West, Rihanna,
Rick Rose na wengine wengi.
Kutokana na uwezo wake kuandika nyimbo nzuri na kipaji cha kuimba Hip
Hop na RnB ndiyo unawavutia watu wengi na kumfanya kuwa miongoni mwa
wasanii bora wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye industry ya muziki
duniani.
Justin Bieber
Bieber ni miongoni kati ya wasanii waliopata umaarufu wakiwa na umri
mdogo. Mpaka sasa Bieber ana umri wa miaka 22 lakini ameshafanikiwa
kufanya mambo mengi kwenye industry ya muziki ambayo inamfanya
awemaarufu dunia nzima.
Pia Bieber amefanikiwa kupata tuzo kibao zikiwemo za Billboard Music
Award, Grammy Award, MTV European Music Award na nyingine nyingi.
Bieber amefanikiwa kuachia albamu nne mpaka sasa, ‘My World 2.0’ mwaka
2009, ‘Under The Mistletoe’ mwaka 2011, ‘Believe’ mwaka 2012 na
‘Purpose’ Novemba 2015. Albumu yake ya nne ilifanikiwa kuuza kopi
milioni 44.7 kwa nchi ya Marekani na iliuza kopi milioni 75 kwa dunia
nzima, pia imefanikiwa kuingia kwenye list ya kuwa ni mwa albumu
zilizouza kopi nyingi duniani.
Justin Bierber amefanikiwa kuingia kwenye top ten ya Forbes Magazine kwa
mara tatu mfululizo kama ‘Most Powerful Celebrities’. Pia amewahi kuwa
msanii wa kwanza video yake kupata views bilioni kumi kwenye Vevo.
Japo amekuwa ni msanii mwenye vituko vingi kwa kipindi cha nyuma na
kupelekea kuachana na mpenzi wake, Selena Gomez ilionekana kuwa ulikuwa
ni utoto lakini kwa sasa ameonekana amebadilika kuja kwa vingine
akianzia kwenye wimbo wake wa ‘Sorry’ uliofanikiwa kupata views zaidi ya
bilioni moja na milioni 218 na bado anaendelea kufanya vizuri.
0 comments:
Post a Comment