Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Ukombozi manispaa ya Singida, Samwel Juma Kingu
(47), amekamatwa na TAKUKURU kwa madai ya kuomba rushwa na baadae
kutiwa nguvuni akiwa ndani ya nyumba ya wageni.
Mtuhumiwa
Kingu anakabiliwa na makosa mawili ya kushawishi/kuomba rushwa ya ngono
na kosa la pili ni kujaribu kupewa rushwa ya ngono wakiwa kwenye nyumba
ya kulala wageni.
Mwalimu
mkuu huyo wa shule ya msingi, alikuwa akiomba rushwa hiyo kwa mwanamke
ambaye Februari, 17 mwaka huu alifika shuleni hapo kumwombea uhamisho
mdogo wake wa kiume.
Mwanafunzi huo wa darasa la sita, alikuwa anaomba kuhamia Temeke jijini Dar-es-salaa kuendelea na masomo.
Mkuu
wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Joshua Msuya, alisema mtuhumiwa huyo
amekamatwa Aprili, 5 mwaka huu saa 10 jioni, akiwa ndani ya nyumba ya
kulala wageni J.M Ferama chumba kilichopewa jina la simba.
Alisema
mwanamke huyo alimwomba kwa muda mrefu uhamisho huo na ndipo mkuu huyo,
aliweza kumpa sharti kwamba wafanye mapenzi kwanza ndipo ampatie
uhamisho huo.
“Baada
ya hapo, mwanamke huyo alifika ofisini kwetu na kueleza jinsi
alivyokuwa akiombwa rushwa ya ngono kwa ajili ya uhamisho wa mdogo wake,
tuliweza kuweka mtego na kufanikiwa kumnasa akiwa mtupu akisubiri
mwanamke naye avue nguo ili atimize azima yake,” alisema.
Msuya alisema kwa sasa wanaendelea kumhoji na upelelezi ukimalizika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
chanzo>dewjiblog
0 comments:
Post a Comment