Mchezo
wa mapema leo Jumamosi wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya West Ham United
iliyoikaribisha Arsenal umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya goli
tatu kwa tatu.
Arsenal
ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia Mesut Ozil dakika ya 18 na
baadae Alexis Sanchez kuongeza la pili ambapo baada ya hapo Andy Carroll
aliisawazishia timu yake magoli yote mawili dakika ya 44 na 45 na
wakaenda mapumziko wakiwa wamefungana goli mbili kwa mbili.
Kipindi
cha pili katika dakika ya 52, Andy Carroll kwa mara nyingine aliongeza
goli la tatu kwa upande wa West Ham na baadae dakika ya 70, Laurent
Koscielny akaifungia goli la tatu Arsenal na mchezo huo kumalika kwa
sare ya goli tatu kwa tatu.
Baada
ya matokeo hayo, Arsenal imefikisha alama 59 ikiwa katika nafasi ya
tatu na West Ham kufikisha alama 52 ikiwa nafasi ya sita ya msimamo wa
Ligi Kuu ya Uingereza.
0 comments:
Post a Comment