Yanga imeondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabo 3-2 hiyo ni baada ya jana kufungwa bao la usiku na kupoteza mchezo kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria nchini Misri.
Mara baada ya mchezo huo ambao wachezaji wa Yanga walipambana kwa nguvu zote mwanzo mwisho, baadhi yao waliangua kilio mara baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha mwisho kutokana na kazi kubwa waliyoifanya kuvurugika dakika za lala salama.Ah Ahly ndiyo walikuwa kupata bao lakini Yanga wakasawazisha kupitia kwa Donald Ngoma ambaye alifunga kwa kichwa baada ya kuunganisha pasi nzuri ya beki wa kulia Juma Abdul.
Beki wa kushoto wa Yanga, Oscar Joshua hakuamini macho yake na alikuwa mmoja wa wachezaji walioangua kilio mara baada ya mwamuzi kupuliza kipenga kwa kuwa waliamini mchezo huo ungemalizika kwa sare ya bao 1-1 kisha kuongezwa dakika 30.
Mpaka kufikia dakika ya 90 matokeo yalikuwa 1-1, mwamuzi wa akiba akonyesha kuwa kuna dakika 5 za nyongeza, wakati huo kwenye benchi la Al Ahly wote walikuwa katika hali ya taharuki huku wakiwa hawaamini kilichokuwa kikitokea uwanjani.
Wakati ikionekana sasa mwamuzi anajiandaa kumaliza mchezo ndopo bao hili likaingia na wachezaji kujikuta wakianza kulia, kiungo Thaban Kamusoko aliwaongoza katika kuwatuliza.
Yanga sasa itashiriki katika mechi za mtoano za Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa.
0 comments:
Post a Comment