Lile jina alilowahi kubatizwa Mwanamke kuwa ni “PAMBO LA MJI” Kwa sasa imekuwa kinyume na badala yake anaandamwa na majukumu lukuki likiwemo la Sokoni,
Kupika, Kulima, Ufugaji, Kumuandaa mtoto, Kuteka maji, Usafi,
Kumliwaza mume, Kulea, Biashara ndogondogo, Kunyonyesha na mengine
mengi. Hatakama haitawezekana
kusaidiwa baadhi ya majuku hayo kwa kigezo cha 50/ 50 basi mwanamke
hufarijika anapofanyiwa mambo haya ingawa wanaume wengi huchukulia
kawaida.
Mwanasaikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Chris
Mauki kuhusu jambo gani mwanamke hufarijika anapofanyiwa licha ya
kuelemewa na majukumu lukuki, ambapo amelitaja swala la Mawasiliano kuwa
ni moja ya vitu ambavyo wanawake wanapenda ingawa wanaume wengi
wanashindwa kutekeleza hilo suala kwa kuona halina umuhimu.
“Wanawake
wanapenda mawasiliano wanapenda uwasiliane wajue uko wapi unafanya
nini, na nani, wanaume wengi wakishaulizwa maswali kama haya wanakuwa
wakali, kuna mahitaji ambayo wote wanafanana na kuna vile wanavyovipenda
kama kuambiwa ukweli lakini mwingine anakataa mimi bora asiniambie”
Wanawake wanapenda ukaribu wa kujali
hisia zake, kuzungumza nae kuonyesha unamjali, kuonyesha una muamini na
kumpa kipaumbele katika maisha ya kawaida hata kwenye mahusiano, vile
vile mwanamke anapenda kujaliwa katika matatizo na kusifiwa pale
anapopatia au anapofanya kitu sahihi hii pia ni katika maisha ya mapenzi
na hata nje ya mapenzi.
Katika mahusiano mwanamke anapenda
kuhakikishiwa ulinzi na usalama wake kiafya, kihisia na kiuchumi pia
mazungumzo ni muhimu kwa sababu mwanamke huumizwa sana na vipindi virefu
vya ukimya sio tu kwamba wanataka mazungumzo bali mazungumzo yenye
kuleta hamasa katika maisha na yenye mvuto ndani yake, alisema Mauki.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment