Mtunzi: Enea Faidy
Ilipoishia sehemu ya kwanza ( kama hukuisoma bofya hapa)
.....Wakati
wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke
yake nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na Giza totoro. Alikuwa
uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku
akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe....
Sehemu ya pili
...DOREEN aliendelea kuongea maneno aliyoyajua mwenyewe akiwa bado yupo uchi wa mnyama nyuma ya bweni alilokuwa anaishi.
Ghafla
kipande kidogo cha karatasi nyeupe kikashuka mikononi mwake bila
kuonekana kilikotokea. Doreen alicheka kwa sauti Kali ya kutisha sana
kisha akalikazia macho karatasi lile, matone ya damu yaliangukia kwenye
karatasi lile kutoka kwenye macho yaliyotisha sana ya Doreen kwani
yalikuwa na rangi nyeusi halafu yakawa na umbile kama macho ya paka.
"Nenda
mpaka ofisi ya mkuu wa shule ukamalize kazi." alisema Doreen akiwa
amelinyanyua karatasi like kwa mkono wake wa kushoto. Karatasi
likatoweka mkononi mwake na kupepea kwa nguvu kama vile limerushwa na
upepo mkali.
Doreen
alipomaliza kazi hiyo akasimama vizuri kama mwanajeshi aliyejipanga
kwaajili ya gwaride kisha akainamisha kichwa chake chini akapotea eneo
lile.
0 comments:
Post a Comment